Kabla ya serikali kujenga kituo hicho cha afya kwenye kata ya Kitumbeine, wakazi wa vijiji vya eneo hilo walikuwa wanalazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 60 ili kupata huduma za afya, katika hospitali ya wilaya iliyopo mjini Longido.
Mfalme Charles III ana siri yake moja. Anaupenda mti mkubwa wa Mkuyu ulioko chini ya Maporomoko ya Maji ya Tululusia, katika hifadhi ya Taifa ya Arusha, Tanzania
Faru walioko kwenye mradi maalum katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Mkoani Kilimanjaro, wanaendelea kuongezeka na sasa Grumeti, ambaye ni mnyama pendwa wa Mwana wa Mfalme wa Uingereza, amepata mjukuu
Wataalam wanaonya kuwa mimea vamizi inayochipuka kwa kasi chini ya Mlima Meru sasa inatishia uoto wa asili pamoja na wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Arusha