Laiti kama wanyama nao wangetakiwa kuwa na vitambulisho basi Paka wasingesajili kwa kutumia alama za vidole.
Paka hasa angesaini kwa kukandamiza pua yake. Hii ni kwa sababu alama ya pua ndio hutofautisha paka mmoja baina ya mwingine.
Kupitia pua zao ndio utapata upekee wa kila paka duniani
Paka wengi ni mashoto kwa maana ya kwamba miguu yao ya kushoto ndio hutawala katika shughuli zao nyingi.
Mara nyingi paka ni wapole hawapigani kwa ajili ya kuonyesha umwamba wao ukimuona paka anapigana ujue anapigania haki yake hasahasa kulinda himaya yake.
Watu wa zamani kule Misri walikuwa wakinyoa nyusi zao ilikuonyesha majonzi Iwapo paka wao wa nyumbani atafariki.
Uwezo wa paka kunusa ni mara 14 zaidi ya uwezo wa binadamu.
Paka pia anaweza kuruka hadi futi nane (8) kwenda juu. Mnyama huyu anaweza kuruka mara sita ya urefu wa mwili wake.
Paka ana akili nyingi kuliko mbwa.
Hii ni kwa sababu paka ana zaidi ya neurons million 300 wakati mbwa ana neurons million 160 huku binadamu akiwa na zaidi ya neurons bilioni 80.
Ikumbukwe pia kuwa hizo neurons bilioni 80 kwa binadamu ni asilimia Kati ya 10-20 tu ya akili ya mtu kamilifu.

Paka anaweza kuishi hadi miaka 30. Hadi sasa paka anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuishi umri mrefu ni Paka Creme Puff aliyeishi miaka 38 na siku tatu. Paka huyo aliishi katika jimbo la Texas nchini marekani.
Paka anavyotoa mlio wa ‘Meaows’ huwa ni pale tu anapokuwa anawasiliana na binadamu. Wao peke yao huwa kamwe hawawasiliani kwa kutumia mlio wa “Meaows” au “Nyau!”
Paka huweza kujitibu majeraha kwa kukoroma (purring).
Paka wa nyumbani huweza kuzalisha frequency Kati ya 25 hadi 150 hertz Kwa kiwango hiko kinaweza kusaidia mifupa na misuli kukua vizuri na pia kujitibu yenyewe.
Mapigo ya moyo ya Paka yanapiga mara mbili zaidi ya Mapigo ya moyo ya binadamu.
Kwa Paka ndani ya dakika moja moyo wake hupiga kati ya mara 110 hadi 140.
Kawaida, Moyo wa Binadamu hupiga mara 60 hadi 100 ndani ya dakika moja.
Mwaka 2004 wana Ekolojia kutoka Ufaransa waliweza kugundua kaburi (mifupa) ya paka inayokadiriwa kuwa ni ya zaidi ya miaka 9500 huko nchini Cyprus
Kabla ya hapo ilikuwa inaaminika kuwa wanyama paka walinza kuishi nchini Misri. Ile Misri ya kale.
Paka aitwaye ‘Stubb,’ alishawahi kuwa meya wa Talkeetna kwa miaka 20. Talkeetna ni mji mdogo wa Alaska.
Katika miaka hiyo 20 alikuwa anakosa Mpinzani wa kugombea nae Japo paka huyo Hakuwa anashika madaraka ya kiutawala lakini alikuwa anapendwa tu na watu wa Talkeetna
Paka mrefu zaidi duniani ni Stewie alikuwa na urefu wa inchi 48.5 wakati paka mrefu kwenda juu zaidi duniani ni Arcturus alikuwa na urefu wa kwenda juu wa inchi 19.05
Asilimia 70 ya maisha ya paka wanayatumia kwa kulala (Kwa mfano kama paka ataishi miaka 10 Basi miaka 7 yote ataitumia kwa kulala)
Paka anayeshikilia rekodi ya utajiri zaidi duniani ni Paka Blackie utajiri wa paundi million 7 ambazo kama tutazibadili kwa thamani ya pesa ya Tanzania ya sasa tunaweza kusema kuwa paka huyo alikuwa na zaidi ya utajiri wa Billion 21.
Hata hivyo Paka huyo alirithi utajiri huo kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wake.
Kama hujawahi kumuona Twiga akitembea au kama hujawahi kumuona Ngamia akitembea Basi kamuangalie Paka akitembea.
Inadaiwa kuwa jinsi paka anavyotembea ni sawa na Ngamia anavyotembea.
Mwendo wa paka pia ni kama ule wa Twiga anavyotembea.
Kwahiyo badala ya kumsifia mtoto au mrembo kwamba ana mwendo wa Twiga Unaweza kumwambia tu kuwa ana mwendo wa paka. Ingawa pengine anaweza asifurahie sana.
Kwa asilimia 80 maumbile ya paka yanafanana na Chui Lakini pia baadhi ya tabia za paka pia hufanana na chui.
Waingereza huwaita wanyama kama Simba, Chui na Duma kuwa ni wa jamii ya “Paka!”
Paka ana uwezo wa kukimbia kwa Kasi ya kilometa 30 kwa saa.
Chui yeye ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilometa 40 kwa saa. Inaaminika kuwa Duma yeye huenda zaidi ya Kilometa 110 kwa saaa.
Paka ana mifupa mingi zaidi kuliko binadamu. Idadi yake ikifikia 230 wakati binadamu ana mifupa 206 tu.
Paka anaweza kubeba mimba akiwa na umri wa miezi minne.
Historia inaonesha kuwa Paka alianza kuishi majumbani zaidi ya miaka 3600 BC.
Ajabu nyingine ni kwamba Paka ni mnyama ambaye hatajwi kabisa kwenye Biblia.
Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari