Mawakili wake, Joseph Ole Shangay and Alasi Melau sasa wanafungua kesi katika mahakama kuu kuvishitaki vyombo vya usalama kwa kumshikilia mteja wao kwa Zaidi ya saa 24 bila kumfungulia mashitaka yeyote.
Param Kilimanjaro, iliyoko katika taasisi ya Nelson Mandela, mkoani Arusha inatajwa kuwa ndio kompyuta yenye uwezo mkubwa zaidi katika eneo zima la Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Msajili huyo wa Hazina, serikali imewekeza Zaidi ya Trillioni 73 katika taasisi za umma na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha fedha hizo zinazaa matunda makubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
Tanzania ina waalimu 250,000. Benki ya NMB imedhamiria kuwaokoa kutokana na mikopo ya mitaani, maarufu kama kausha damu ambayo imekuwa ikimaliza mishahara yao.
Maonesho ya 29 ya kilimo kuelekea Sikukuu ya Nanenane 2023 kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika katika viwanja vya Nane-Nane, eneo la Njiro, kusini mwa jiji la Arusha, na yamezinduliwa rasmi na Spika wa Baraza la wawakilishi, Zanzibar Zuberi Ally Maulid.