Tanki la Bohari ya Mafuta lazua Taharuki Dar-es-salaam

Wakazi wa jiji la Dar-es-salaam wamekumbwa na taharuki kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni kuvuja kwa mafuta kwenye tenki kubwa la bohari ya Malawi Cargo Center.

Tukio hilo liliripotiwa siku ya kwanza ya Disemba 2022 kuanzia majira ya saa mbili asubuhi na kuendelea, ambapo taarifa za mitandaoni zilitahadharisha madereva kutokupita eneo hilo.

Hata hivyo taarifa kutoka mamlaka husika zinadai kuwa bohari la MCCL lilikuwa linapokea mafuta ya jamii ya petroli kutoka kwenye meli ya STI MILWAUKEE kutoka KOJ -1 kiasi cha tani 2048 ikiwa inatazamiwa kukamilika mnamo saa tatu na nusu asubuhi (03:30).

Hata hivyo, wakati wa zoezi la kupokea huku wafanyakazi wa ghala la MCCL wakiendelea kufuatilia mwendendo mzima katika tenki, walionelea kuwa ni muhimu wapooze tenki kutokana na kuongezeka kwa joto.

Katika kuwasiliana na meli waliona tank lao ninaelekea kujaa hivyo kuwasiliana na Loading Master ili kusimamisha meli na kufanya vipimo kujua kama mafuta yaliyopaswa kupokelea ndio yaliyosukumwa na meli.

Kwakuwa tank lilikuwa limejaa waliona ni vema kufungua cooling sprinklers ili kupooza tanki kuzuia mafuta yasiweze kumwagika kwakuwa yalikuwa katika pressure kubwa na joto la juu.

Baada ya meli kusimama majira ya saa tatu na dakika thelasini na sita (03:36) vipimo kutoka melini vilionyesha mafuta yaliyosukumwa kutoka melini ni kiasi cha tani 2013.72 pungufu ya tani 35 zilizotarajiwa.

Baada ya PBPA kupata taarifa ya hali ya taharuki ilituma Surveyors wake mara moja kwenye ghala husika ili kujiridhisha na taarifa hizo.

Katika ukaguzi ilionyesha kuwa hakukuwa na mafuta yaliyomwagika kutoka katika tanki husika bali baada ya kuona kuna hatari ya mafuta kumwagika Terminal Manager alikata seal na kufungua valve.

Hii ni ili kupunguza kiasi cha mafuta katika tank hilo kwa kujaza mafuta hayo katika gari na pia kufungua water cooling system (cooling sprinklers) ili kupunguza joto katika tank husika.

Petroleum Bulk Procurement System inaendelea kufanya uhakiki wa kiasi cha mafuta yaliyopokelewa katika ghala la MCCL, kiasi cha uwezo wa kupokea mafuta walichokuwanacho kabla ya kuanza kupokea na kiasi cha mafuta kilichojazwa katika gari husika.

Hivyo tunapenda kukujulisha kuwa hakuna mafuta yeyote yaliyomwagika katika ghala la MCCL bali maji yaliyokuwa yakipooza tank ndio yalileta taharuki kwa Umma.

Maoni yamefungwa, lakini 0naweza kushea habari