Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Ligi Kuu Hispania Yajitosa Michuano ya Soka la Vijana Afrika Mashariki 2022

Nyota Ndogo kutoka Kenya nao watakuwepo

Timu za vijana kutoka nchi za Uarabuni na Marekani kwa mara ya kwanza mwaka huu zitashiriki katika michuano ya Afrika Mashariki, maarufu kama Chipkizi Cup.

Na kwa mara ya kwanza pia, ligi ya Uhispania, yaani LaLiga itahusika katika maandalizi ya mashindano hayo yatakoyokuwa makubwa Zaidi mwaka huu, ambapo Zaidi ya timu 220 za soka la vijana Kutoka nchi mbali mbali zimethibitisha kushiriki.

Michuano ya Kombe la Chipkizi Afrika Mashariki msimu wa 13 inatarajiwa kufanyika jijini Arusha, kwa siku sita kuanzia Desemba 13 Hadi 18 mwaka huu.

Michuano hiyo inaandaliwa  na Taasisi ya kuibua na kukuza vipaji iitwayo Future Stars Academy yenye makao yake makuu Jijini Arusha.

Alfred Itaeli ambaye ni mkurugenzi wa taasisi hiyo amethibitisha kuwa michuano yam waka huu inaungwa mkono na Ligi ya Taifa ya Hispania (LaLiga) huku ikizikutanisha timu kutoka nchi 10 duniani zikiwemo nane kutoka Afrika.

Mkurugenzi wa Future Stars Academy, Alfred Itaeli, anaongeza kuwa ‘Chipkiz Cup’ imevutia zaidi ya timu 200 kutoka nchi za Falme za Kiarabu, Marekani, Somalia, Cameroon, Zimbabwe na Nigeria ambao watashiriki Kwa mara ya kwanza.

” Timu Kutoka nchi hizo zimeshathibitisha kushiriki na wanasubiri ratiba pekee ya kuja kushindana ambao zitaungana na timu wenyewe za Afrika mashariki Kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi Zanzibar na Tanzania”

Alisema maandalizi yote kuelekea Mashindano hayo yamekamilika, huku wakimalizia kurepea viwanja watakavyotumia ikiwemo sheikh amri abeid na za shule za kimataifa zilizoko Arusha ambapo Mashindano yatashirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka saba, 9, 11, 13, 15, 17, 20 na Wasichana chini ya miaka 11, 15 na 20.

Jorge Gazapo ni balozi wa Maendeleo ya michezo, Kimataifa anayewakilisha LaLiga katika nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi ambaye anasema ligi kuu ya Hispania imeweka mbele suala la kuwainua vijana katika soka.

“Na ndio maana tupo hapa tukijiandaa kushiriki ipasavyo katika mashindano ya Chipkizi Cup,” anasema Jorge Gazapo.

Balozi huyo anaongeza kuwa LaLiga inatarajia kuleta baadhi ya makocha kutoka timu za vijana kuja kuvuna vijana watakaoonesha kiwango kizuri Kwa ajili ya kuwaendeleza.

“Kujitolea kwa LaLiga hadi mashinani hakuna shaka, ndiyo sababu kwa sasa tupo Arusha kwani tunaamini kwamba mustakabali wa uendelevu wa soka uko kwa vijana hivyo ushirikiano huu tumeanza kwenye Mashindano haya Kwa ajili ya kuwapa vijana wa Tanzania uwanja mpana wa kucheza soka la kulipwa nje kupitia chipkizi cup,” alisema.

Kwa Upande wake katibu wa chama Cha soma mkoa wa Arusha, Emmanuel Anthony alisema kuwa watashirikiana na waandaji kuhakikisha Mashindano yanafanikiwa Kwa manufaa ya soka la Arusha na Taifa kwa ujumla.