Wanasheria wa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Shangai ambaye ametoweka katika mazingira ya kutatanishia kutoka kituo cha polisi alichokuwa anashikiliwa wilayani Karatu, wako mbioni kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mawakili wake, Joseph Ole Shangay and Alasi Melau sasa wanafungua kesi katika mahakama kuu kuvishitaki vyombo vya usalama kwa kumshikilia mteja wao kwa Zaidi ya saa 24 bila kumfungulia mashitaka yeyote.
Mbunge Shangai ni mmoja wa wakazi Zaidi ya 31 waliokamatwa na Polisi hivi karibuni wilayani Ngorongoro kwa tuhuma mbalimbali ambazo kwa sasa bado ni vigumu kuziainisha.
Lakini Mbunge huyo wa Ngorongoro Emmanuel Shangai, yeyeye alikamatwa akiwa safarini kutokea Arusha, alikokwenda kuripoti katika kwa mkuu wa upelelezi (RCO) katika Makao makuu ya Polisi.
Hata hivyo RCO aliwaagiza kurejea tena Ngorongoro lakini wapiti Karatu ambako wangeripoti katika kituo cha polisi cha wilaya hiyo.
Wakiwa njiani gari la mbunge huyo na mawakili wake lilizuiwa eneo la Rhotia na watu waliojitambulisha kuwa ni askari, wakiwa na magari mawili.
Baada ya hapo, Mbunge huyo na wakili wake Joseph Oleshangay walipelekwa katika kituo cha polisi cha Karatu ambako kwa mujibu wa wanasheria wake, alihojiwa kwa Zaidi ya saa 6 na kulazimika kubaki kituoni hapo hadi asubuhi.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kupeleka maombi ya kufungua kesi hiyo Mahakamani,mawakili wa mbunge huyo walisema tangu akamatwe juzi hawajuwi alipo.
Wakili Joseph Oleshangay amesema wameamua kwenda Mahakamani ili kupata Haki kwani makosa ambayo mbunge huyo na wananchi wengine wanashitakiwa yanadhamana.
“Mbunge pamoja na wananchi wengine zaidi ya 30 ambao wanashikiliwa na polisi wote wanatuhumiwa kwa kosa Moja la kujeruhi ambalo linadhamana”amesema
Amesema juzi baada ya mbunge kukamatwa yeye alikuwa naye na polisi walimuahidi angepata dhamana Jana lakini Hadi Leo bado hajapata dhamana na hawajuwi alipo.
“Siku ule usiku pale Karatu baada ya kuandika Maelezo niliwaomba wadhamana polisi wakaniambia Jana angepata lakini baada ya kurudi asubuhi sinamkuta polisi tukaelezwa ameletwa Arusha ambapo Hadi Leo hatujuwi alipo”amesema
Wakili mwingine Alais Melau amesema pia wanataka Watuhumiwa wote wafikishwe Mahakamani kwani makosa Yao wanadhamana.
“Tupeleka maombi ya kesi kwa msajili tunaimani kesi itapangiwa Hakimu wa kusikilizwa haraka uwezekavyo ili haki ijulikane”amesema
Amesema wananchi waliokamatwa tangu Agosti 17 baadhi Hali zao ni mbaya kutokana na vipigo na wengine ni wagonjwa”amesema
Hata hivyo,bado Jeshi la polisi mkoa Arusha halijatoa taarifa alipombunge Oleshangay na jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoa Justin Masejo zinaendelea.