Singida na Morogoro
Mikoa hii miwili ndio inayoongoza kwa kuwa na majirani wengi au kwa kupakana na mikoa mingine mingi zaidi nchini Tanzania.
Mkoa wa Singida unapakana na mikoa mingine nane, na Morogoro pia hupakana na mikoa mingine minane, ingawa Singida na Morogoro yenyewe haipakani.

Mkoa wa Morogoro unapakana na mikoa ya Pwani, Lindi, Ruvuma, Njombe, Tanga, Dodoma, Manyara na Iringa, jumla ikiwa ni mikoa nane kama tulivyoona awali.
Morogoro pia ndio mkoa mrefu Zaidi kuliko yote nchini Tanzania.
Singida wenyewe unapakana na mikoa ya Manyara, Arusha, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Mbeya, Iringa na Dodoma, hii pia ikiwa ni mikoa nane.
Tabora
Mkoa wa Tabora ndio mpana Zaidi nchini, huku ukiwa umepakana na mikoa mingine sita.
Tabora pia ndio mkoa mkubwa Tanzania kwa eneo.
Dar-es-salaam
Sasa pia kuna mkoa unaoongoza kwa kuwa na majirani wachache, na huu ni mkoa wa Dar-es-salaam ambao unapaka na mkoa mwingine mmoja to, Mkoa wa pwani, basi.
Lakini pia mkoa wa Dar-es-salaam ndio Mkoa mdogo kuliko mikoa yote Tanzania.
Cha ajabu ni kwamba, Dar-es-salaam, pamoja na udogo wake na pia kukosa majirani, ndio mkoa wenye idadi kubwa ya watu kuliko mikoa yote nchini.
Dar-es-salaam unakadiriwa kuwa na wakazi Zaidi ya Milioni Sita. Hii ni takribani asilimia moja ya watanzania wote wanaishi Dar-es-salaam.
Wakati wa mchana idadi ya watu wa Dar-es-salaam huongezeka mara mbili.
Dar es salaam ndio Mkoa unaoongoza kwa kuwa, na watu wengi wakati wa mchana kuliko mikoa yote Tanzania.
Watu wengi wanaoonekana jijini Dar-es-salaam na viunga vyake nyakati za mchana huwa wanatokea maeneo ya jirani, hasa nje ya mkoa.
Wengi wanatokea mikoa ya Pwani, Tanga, Zanzibar, Dodoma na Morogoro. Na asilimia kubwa hufika jijini humo na kuondoka nyakati za jioni.
Dar-es-salaam pia ndio mkoa unaoongoza kwa uhalifu na visa vya utapeli nchini.
Kwa upande wa hali ya hewa mkoa wa Dar es salaam ndio unaoongoza, kwa joto.
Njombe na Mbeya
Mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na baridi kali zaidi Tanzania.
Mkoa wa Mbeya nao ukiongoza kwa wingi wa mvua nchini.
Kigoma ndio mkoa ambao jua hukawia kuzama na vile vile kukawika kuchomoza.
Arusha
Mkoa wa Arusha unaogoza kwa kuwa na milima au vilima vingi.
Na pia ndio mkoa wenye mpaka mrefu zaidi na nchi ya Jirani. Kuna zaidi ya kilometa 500 ambazo Arusha hupakana na Kenya upande wa kaskazini.
Arusha pia ndio eneo ambalo wakazi wake ni wataalamu wa kufanya biashara, huku Mkoa wa Mtwara ukiwa unaogoza kwa watu wake kutokujua kufanya biashara.
Kilimanjaro
Kilimanjaro ndio mkoa pekee wenye hali zote za hewa na mandhari tofauti ya nchi.
Kwanza kilele kirefu zaidi barani Afrika, kipo Kilimanjaro.
Misitu minene pia hupatikana Kilimanjaro, ukiwemo mti mrefu kupita yote na miti yenye umri mkubwa zaidi.
Maeneo ya nusu jangwa pia yapo Kilimanjaro, Maziwa na Mito mingi pia ipo Kilimanjaro, miinuko na Tambarare bila kusahau joto na baridi kwa wakati mmoja.