Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Safari katika Hifadhi ya Ziwa Manyara

Hifadhi ya taifa ya ziwa manyara ilipata jina lake kutoka na mmea uitwao ‘Mnyaa.’

Ambao kwa lugha ya kimasai unajulikana kama emanyara wamasai hutumia mmea huo kutengenezea uzio wa boma.

Ziwa Manyara hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya taifa mwaka 1960 ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya Serengeti.

Manyara iliandikishwa na umoja wa mataifa kama usitiri wa maisha mnamo mwaka 1981.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 648.7 kati ya hizo kilomita 386 ni eneo la ziwa.

Hifadhi ya Ziwa manyara ipo kaskazini mwa Tanzania umbali wa kilomita 115 magharibi mwa jiji la arusha kando ya barabara ya makuyuni-ngorongoro karibu na mjimdogo wamto wa mbuu.

Wakati mzuri wa kutembelea Hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara ni Katika miezi ya juni mpaka oktoba  ni wakati mzuri wakuona wanyama wakubwa  wakati machi hadi mei unaweza kuona ndegena utalli wa kupiga makasia majini na pia kipindi hichi Hifadhi huwa na mandhari ya kupendeza.

Unapoanza kuingia hifadhini unakutana na uoto wa misitu wa asili wa maji ya aridhini wenye miti mirefu ambayo ni makazi ya nyani na kima.

Baada ya msitu huo unakuta msitu wa migunga, vichaka, mbuga za nyaasi fupi na tindiga.

Kwa nini watalii hutembelea mbuga ya ziwa manyara

Watalii hupenda kutembelea Hifadhi hiyo kwa sababu Hifadhi ya taifa ya ziwa manyara ipo pemebezoni mwa barabara kuu iendayo kwenye Hifadhi maarufu kama Serengeti na Ngorongoro.

Pia ina vivutio ambavyo havipatikani ndani ya Hifadhi nyingine yoyote kama vile maji moto, msitu wa majia ya aridhini pamoja na ukuta wa bonde la ufa, vivutio vingine vinapatikana ndani ya Hifadhi kilomita 50 tu na ni rahisi kufikika Katika kipindi chote cha mwaka.

Simba hupanda miti Katika Hifadhi zingine lakini ni rahisi kuwaona katika Hifadhi ya taifa ya ziwa manyara kutoka na mazingira ya Hifadhi.

Pia uwepo wa kijiji maarafu cha mto wa mbuu ambacho husifika kwa kuwa na makabila zaidi ya 120 yanayo patikana nchini Tanzania.

Aina ya vivutio vinavyopatikana Katika ziwa manyara

Wingi wa aina ya wanyama na makazi yao yapatoyo saba ndani ya eneo dogo, ziwa lenye mandhari ya kupendeza na ni makazi ya makundi makubwa ya ndege aina ya heroe, simba wakweo miti, makundi makubwa ya tembo na nyati, msitu wa maja ya aridhni pamoja na ukuta wa bonde la ufa.

Pia kuna msitu wa murang ambao hupatikana aina mbalimbali za ndege na mimea mbalimbali, aina za ndege mbalimbali zaidi ya aina 390 wahamao na wakazi, bwawa la viboko pamoja na chemchem ya maji moto.

Hii chemchem ya Maji Moto hupendwa sana na watalii wa kitanzania, wengi wakiamini kuwa maji hayo yana nguvu za ziada za kuondoa magonjwa na mikosi.

Msitu wa Murang’

Msitu huu upokusin mgharibi mwa Hifadhi Katika mlima wa mbulu.msitu huu una ukubwa wakilomita za mraba 230.6 na upo ukanda wa juu wa miteremko wa bonde la ufa.

Msitu wa murang ni makazi ya jamii mbalimbali za wanyama akama vile temb, nyati, swala wadogo na jamii za ndege wa misituni kama vile hondo hondo, tai na mwewe na pia na jamii ya miti kama vile mtakahiko, loliondo, mfuruanji, na mkuyu.

Shughuli za kitalii zinazofanyika Katika msitu wa murang ni kupiga kambi maalum kuangalia baadhi ya ndege na matembezi ya miguu.

Jukwaa jipya la kutizamia wanyamaa na ndege la mbao lenye urefu wa futi 8 kutoka usawa wa aridhi. Jukwaa hili liko umbali wa kilomita 8 kutoka lango kuu la kuingilia hifadhini.

Ukiwa juu ya jukwaa hili unaweza kuona kwa uakaribu eneo evu ambalo ni makazi ya ndege maji na wanyama akama viboko, nyati , nyumbu na pundamilia.

Daraja la kamba ni njia ya kutembea juu ya daraja ni draja la kwanza la kutembea kwa miguu nchini tanzania na refu kuliko yote afrika.

Njia hii hukupa fursa ya kutizama vivutio vyote vinavyokuzunguka kutokea juu.

Yaani unafurahia maisha juu ya miti ikiwa inakuzunguka na vipepeo, nyani na ndege.

Daraja hili la kamba Katika miti lina urefu wa mita 400 na huanza kwa kutembea juu ya mbao fupi na kukwea kwa taratibu kwa kutokea usawa wa aridhi hufikia kimo cha mita 18 kutokea aridhini.

Matembezi juu ya daraja yanayounganishwa na miti hukupa hisia za kutembea juu ya miti.

Malazi ndani ya Hifadhi kuna mabanda, kambi za kupiga mahemu hostel ya wanafunzi na hotel iitwayo lake manyara tree lodge.

Kanuni na taratibu za Hifadhi wageni wanakumbusha kwamba ni kosa kusumbua wanyama, kupiga makelele kama honi, kupiga muziki kwa sauti kubwa au usumbufu mwingine wowote kwa wageni wengine.

Ni kosa kuingiza mmea ndani ya Hifadhi kuchuma au kuharibu uoto wa asili.

Kusababisha moto ndani ya Hifadhi, kuingiza wanyama wafugwao ndani ya Hifadhi, kuendesha mwendo wa kilomita 50 zaidi ndani ya Hifadhi, kutoka njee ya gari tofauti na sehemu inayoruhusiwa,

Au kuingia na silaha ya aina yoyote ndani ya Hifadhi.

Pia unapaswa kukumbuka kwamba kuwa ndani ya Hifadhi kabla ya saa 12:00 asubuhi na baada ya saa 12:00 ni kosa, isipokuwa tuu kwa maeneo ya kulala wageni yanayotambulika.

Mwaka 2022 wapenzi fulani waliamua kufunga ndoa ndani ya hifadhi ya Manyara na hili lilikuwa tukio adimu la kimataifa.