Miaka michache ijayo Afrika itameguka na kujigawa mara mbili ambapo bara jipya litajitengeneza.
Tanzania na Kenya zitakuwa miongoni mwa nchi zitakazounda bara jipya ambalo jina lake litajulikana wakati huo.
Hii ni kwa sababu kuna ufa mkubwa mrefu unaoendelea kujitokeza kuukata upande wa mashariki pamoja na pembe ya Afrika.
Bara la afrika, ni mojawapo kati ya mabara saba, likiwa na nchi 55, huku ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo Milioni 30.4.
Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani baada ya Asia.
Sasa kutokana na ufa mrefu mpana ulioanza kujitokeza Zaidi ya miaka mitano iliyopita na kuendelea kutanuka kipindi hiki, waanasayansi wamethibitisha kuwa hivi karibuni kutazaliwa bahari mpya na bara jipya litakalojitenga kutoka Afrika.
Ufa huo mkubwa ambao umejitokeza na unaendelea kukua ulianzia kusini magharibi mwa nchi ya kenya.

Kupasuka kwa ufa huo ardhini, ukitishia kuligawa bara la afrika uliwafikirisha sana wataalam wa miamba.
Ikumbukwe kuwa wana Jiolojia wanaelezea kuwa zamani sana ardhi yote ya dunia ilikuwa imeungana na kutengeneza bara moja lililojulikana kama Pangea.
Yaani dunia ilikuwa na sehemu mbili tu. Ardhi ya nchi kavu na eneo la maji.
Hata hivyo nyufa kama hizi zinazodaiwa kutokana na mvutano wa miamba katika msingi wa tufe la dunia (Tectonic Movement na tectonic activities) vilisababisha vipande vya ardhi ya juu kutengana.
Matikeo yake ile Pangea ikawa inameguka na baada ya miaka mingi, na kwa nyakati tofauti kukazaliwa mabara saba tofauti na katikati yao kukaibuka bahari saba, au nane.
Mara nyingi vipande vya ardhi huwa vinatengena, kwa kusogea au kutembea katika ulekeo tofauti, ambapo, ambapo hiyo usababishwa na nguvu asilia au natural forces.
Na kwa sasa mvutano mpya wa ardhi unaenedelea kufanyika mashariki mwa bara la Afrika.
Na umeibuka ufa huu mpya ambao unaendelea kutanuka pande zote.
Unajongea upande wa kaskazini, yaani kuelekea nchini Ethiopia na pia kuambaa muelekeo wa Kusini ukisogea zaidi kuelekea Zimbabwe.
Unazigawa tabaka za juu za Somali na Nubian Plates.
Hizo zikiishwa kutenganishwa inatabiriwa kuwa bahari mpya itaibuka hapo katikati.
Halafu sasa bara jipya, litazaliwa ambapo Tanzania, Kenya, Somalia, Malawi, Zambia na Zimbabwe zitajikuta zikiwa nje ya Afrika na katika bara hilo jipya.
Na si ajabu pia ikiwa bara litakalojitenga litasogea mashariki Zaidi ya Bahari ya Hindi kiasi cha kuwa karibu Zaidi na visiwa vya Unguja na Pemba, kama sio kujiunga navyo kabisa.