Taifa Tanzania
Taifa Tanzania. Gazeti Huru la Afrika Mashariki linaloandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Ufugaji Samaki: Kati ya Kambale na Sato, Ni Yupi hasa Anayefaa zaidi kwa Biashara?

Kwa mujibu wa wataalamu wa ufugaji samaki, aina hizi mbili za samaki ni bora, isipokuwa katika maeneo machache kama yanavyoainishwa hapa.


Kila samaki ni bora na anafaa kufugwa kibiashara kwa mujibu wa mazingira aliopo ila tunawakumbusha mambo yafuatayo kwa mujibu wa mazingira ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Sato huwa anatumia chakula chenye protein chache 45 hadi 30 tuu hadi unamvuna wakati kambale anatumia protein kubwa 55 hadi 45 tu hadi unamvuna.


Sasa ikumbukwe kuwa kadri protein inavyokua kubwa ndo kadri gharama ya chakula inavyokua kubwa
Sato pia wanatumia chakula kichache sana ukilinganisha na kambale.

Sato mmoja anakula gramu 75 hadi unamvuna wakati Kambale mmoja anakula Kilogramu 1.45 hadi unamvuna.

3. Sato kilo Moja sokoni anauzwa Tsh 10,000 hadi 8,000 kwa bei ya shamba (Farm gate price) wakati kambale kilo moja anauzwa Tsh 3,500 hadi 4,000

4. Sato habagui walaji(Kila mtu anakuka sato bila kudhurika na hakuna ubaguzi wa kimadhehebu) wakati Kambale anabagua madhehebu na mara nyingine kuna watu wana allergy na kambale

5. Siyo kweli kwamba kambale kwa miezi 6 anafikisha Kilo 1 bali kilo moja kambale anafikisha kilo 1 kwa mwaka mmoja na miezi 3 endapo umemlisha vyema kwa ufugaji wa semi-intensive wakati sato kwa ulishaji mzuri anafikisha robo kilo kwa miezi 6 na anafikia ukubwa wa kuliwa

5. Kwa tanzania Kambale wana utitiri wa magonjwa(Mfano: Dropsy(Kuvimba tumbo), crackhead, ngozi kuchubuka n.k) kulinganisha na sato ambaye kwa Tanzania imeripotiwa magonjwa machache ila vifo vinayokea kwa ajili ya uchafu uliyopitiliza wa maji tu

6. Sato hawalani wakiwa bwawani, ila kambale wanakulana kwahiyo unaweza weka samaki 1000 sato ukawakuta wote ila kambale ukawakuta 800 na wanaokula wenzao ni wale ambao wanaitwa na sisi wafanyabiashara kwamba ni Combat type. 

Zingatia: Hakuna samaki duniani aina ya kambale anayeitwa Combat hili ni neno lisilokuwa na mantiki kitaalam.

Kambale tunayemfuga Tanzania ni mmoja tuu (Clarias gariepinus)  na hakuna kambale combat.

Ule u kombat unasababishwa na mazingira kuna wakati upo na kuna wakati unapotea. Ukiwalisha kambale wako vizuri sana hawatakulana ila bwawa lililokosa lishe nzuri na inayostahili hawa combat watapungua